Manchester United na milioni £150

Manchester United wanaandaa dau la pauni milioni 150 kwa ajili ya wachezaji wapya, wakiwamo kipa wa Ajax Jasper Cillessen, 26, mlinzi wa Real Madrid, Sergio Ramos, 29, kiungo wa Bayern Munich, Bastian Schweinsteiger, 30, na mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema, 27.

Hiyo ni katika mipango mizito ya kocha Louis van Gaal katika kujaribu kuimarisha kikosi chake kilichoshika nafasi ya nne kwenye msimu uliomalizika wa ligi kuu.

Liverpool wanatarajia kugongewa mlango kwa mara ya tatu na Manchester Citykwa ajili ya posa ya mshambuliaji wao, Raheem Sterling, 20, ambaye huenda akauzwa kwa pauni milioni 50.

Kocha wa Sunderland, Dick Advocaat yu tayari kuvunja rekodi ya klabu hiyo kwa kumsajili kiungo wa PSV Eindhoven, Georginio Wijnaldum, 24 anayetoka nchini kwao.

Kiungo wa Borussia Dortmund, Ilkay Gundogan, 24, huenda akabaki kwenye klabu hiyo licha ya kutakiwa na klabu kadhaa, zikiwamo Manchester United na Arsenal.

Newcastle wanatarajia kumuuza mpachika mabao wao, Papiss Cisse, 30, baada ya klabu kadhaa za ligi kuu nchini England kuulizia uwezekano wa kumsajili kwa pauni milioni 10, huku mshambuliaji wa Marseille, Florian Thauvin, 22, lakipangwa kuchukua nafasi yake.

Swansea wapo tayari kumuuza kiungo mshambuliaji wa Hispania, Michu, 29, kwa pauni milioni nne tu atakaporudi Wales wiki hii.

Klabu ya soka ya New York City wapo katika mazungumzo na Juventus kwa ajili ya uwezekano wa kumsajili mkongwe wao, Andrea Pirlo, 36.
Manchester City wanatarajia kuomba kumsajili kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere, 23, ikiwa watashindwa kumpata yule wa Juventus, Paul Pogba, 22.

Liverpool wapo katika hatua nzuri ya kumsajili kiungo wa Barcelona, Gerard Deulofeu, 21, huku Everton nao wakiwa kwenye mchakato wa kumpata, kwa kuwa alikuwa kwao kwa mkopo.

Comments