Ratiba Ligi Kuu England yatolewa 2015/16

*Chelsea wanaanzia nyumbani

Msimu mpya wa Ligi Kuu ya England (EPL) utaanza wiki mja mapema kuliko mwaka jana. Utaanza wiki moja na Football League.

Ratiba ya Ligi Kuu ya England imetoka, ambapo mabingwa Chelsea, wanaanza kutetea ubingwa wao kwa kuwakaribisha Swansea.

Hiyo itakuwa wikiendi ya Agosti 8 na 9 mwaka huu, msimu mpya utakapoanza wakati Manchester City waliomaliza pointi nane nyuma ya Chelsea watasafiri hadi kwa West Bromwich Albion.

Mechi kumi za mwanzo wa msimu 2015/16-EPL
Mechi kumi za mwanzo wa msimu 2015/16-EPL

Arsenal waliomaliza katika nafasi ya tatu wataanza na West Ham wakati waliokuwa wa nne, Manchester United watakabiliana na Tottenham Hotspur katika dimba la Old Trafford.

Liverpool wasiojulikana kama bado watakuwa na Raheem Sterling watapepetana na Stoke, huku Newcastle wakitoana jasho na Southampton wakati Leicester watawakaribisha Sunderland.

Vijana waliopanda daraja msimu huu – Bournemouth, Watford na Norwich watakabiliana na Aston Villa, Everton na Crystal Palace kwa mtiririko huo.

Comments