Pistorious kuachiwa Agosti

Mwanariadha maarufu mwenye ulemavu wa miguu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius anatarajiwa kutoka jela Agosti mwaka huu.

Ushauri huo umetolewa na mamlaka za jela za Afrika Kusini baada ya mchezaji huyo kutumikia kifungo kwa miezi 10.

Alihukumiwa kwenda jela kwa miaka mitano Septemba mwaka jana baada ya kutiwa hatiani kwa kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp.

Wazazi wa Steenkamp, hata hivyo, wanapinga hatua hiyo inayofikiriwa kuchukuliwa kuanzia Agosti 21, wakieleza kwamba muda aliotumikia si sawa na kitendo cha kutoa uhai wa mtu.

Pistorius alijitetea mahakamani kwamba hakumuua kwa kukusudia, bali alifyatua risasi akidhani alikuwa amevamiwa.

Jaji Thokozile Masipa wa Mahakama Kuu ya Afrika Kusini baada ya kutafakari maelezo ya upande wa mashitaka uliodai aliua kwa kukusudia na utetezi, alifikia uamuzi kwamba Postorius hakuua kwa kukusudia.

Wazazi wa Steenkamp, hata hivyo, wanapinga hatua hiyo inayofikiriwa kuchukuliwa kuanzia Agosti 21, wakieleza kwamba muda aliotumikia si sawa na kitendo cha kutoa uhai wa mtu
Wazazi wa Steenkamp, hata hivyo, wanapinga hatua hiyo inayofikiriwa kuchukuliwa kuanzia Agosti 21, wakieleza kwamba muda aliotumikia si sawa na kitendo cha kutoa uhai wa mtu

Hata hivyo, jaji huyo aliamua kwamba Pistorius alitumia vibaya silaha yake kwa kufyatua risasi kupitia mlango ambayo kwa bahati mbaya ilimuua Steenkamp.

Sheria za Afrika Kusini zinatoa fursa kwa mfungwa kama Pistorius kutolewa nje kwa parole lakini abaki chini ya uangalizi madhali ameshatumikia adhabu kwa walau miezi sita.

Kamishna wa Huduma za Mafunzo ya Wafungwa Afrika Kusini, Zach Modise amesema kwamba kamati ya kufuatilia kesi iliyokutana katika Gereza la Kgosi Mampuru II jijini Pretoria aliko Pistorius imeridhika kwamba anatakiwa kutoka jela.

Hata hivyo, hatua hiyo itategemea rufaa inayopendekezwa kupinga pendekezo hilo
Kwa kosa la kuua bila kukusudia, Pistorius angeweza kutupwa jela kwa hadi kipindi cha miaka 15.

Jaji Masipa alisema kwamba Pistorius (27) alichukua hatua haraka mno kufyatua risasi.

Akimsafisha dhidi ya mashitaka ya kuua kwa kukusudia, Jaji Masipa alisema hangeweza kufikiria kuua mtu yeyote aliyekuwa nyuma ya mlango wa maliwato.

Comments