Monk challenges Swansea to take sixth

Swansea wawatibulia Arsenal

 

Bao la dakika za mwisho la Bafetimbi Gomis wa Swansea limemaliza mtiririko wa mechi 11 bila kufungwa wa Arsenal.

 

Wakicheza nyumbani, vijana wa Arsene Wenger wameshindwa kufikisha pointi sawa na Manchester City ili kufikiria kuelekea nafasi ya pili badala ya tatu waliyomo.

 

Swansea wanaofundishwa na Garry Monk waliwavuruga Arsenal kwa kuweka viungo sita na kuwasababisha washindwe kuvuka kwenda kufunga, hasa katika kipindi cha kwanza na ilikuwa kana kwamba mechi ingemalizika kwa suluhu.

 

Kipa wa zamani wa Arsenal, Lukasz Fabianski naye alikuwa kikwazo kingine kwani alizuia mabao ya wazi yaliyokuwa yatiwe kimiani na Santi Cazorla, Aaron Ramsey na wengine, pale The Gunners waliposhambulia kwa nguvu baada ya kipindi cha kwanza.

 

Wenger amesema kwa jinsi walivyocheza, Arsenal walistahili ushindi na kwamba kufungwa huko ni kwa bahati mbaya.

 

Ilibidi itumike teknolojia ya goli kuthibitisha kwamba mpira wa Gomis ulikuwa umevuka mstari wa goli na kwamba kipa David Ospina aliuondoa ukiwa umeshavuka.

 

Huu ni ushindi wa pili kwa Swansea dhidi ya Arsenal, kwani Novemba waliwachaoa pia 2-1 na inaelekea kuna ugumu kwa Arsenal kuwakabili vijana hao wa Wales.

 

Kikosi cha Arsenal kilikuwa kile kile kilichocheza katika mechi nne zilizopita, jambo ambalo halijafanyika tangu 1994, ambapo Wenger amekuwa akiwabadili kwa sababu mbalimbali.

 

Swansea ni timu ya tatu kushinda nyumbani na ugenini dhidi ya Arsenal na Manchester United katika msimu mmoja, wengine ni West Ham (06-07) na Chelsea (09-10).

 

Arsenal wakiwa na mechi moja zaidi ya wenzao (isipokuwa Sunderland) wanashika nafasi ya tatu kwa pointi zao 70, Chelsea wakiwa nazo 84 na Manchester City 73. Man United wamefikisha 68 wakati Liverpool wanazo 72.

Comments