Bournemouth, Watford kamili EPL

 

*Ubingwa wa EPL waenda Bournemouth

 

Bournemouth waliofanikiwa kutinga Ligi Kuu ya England (EPL) msimu ujao wametwaa ubingwa katika Ligi Daraja la Pili maarufu kama Championships.

 

Bournemouth walicheza vyema Jumamosi hii katika siku ya mwisho ya ligi hiyo, wakipata ushindi mnono wa 3-0 dhidi ya Charlton.

 

Waliokuwa wakipewa nafasi ya ubingwa, Watfrord, waliteleza dhidi ya Sheffield Wednesday kwa kwenda sare.

 

Mabao ya Bournemouth ayalifungwa na Matt Ritchie aliyetia mawili na Harry Arter kuhakikisha ushindi kwa vijana hao wa kocha Eddie Howe.

 

Bournemouth sasa wamemaliza ligi wakiwa na pointi moja mbele ya Watford na timu zote hizo mbili zimepanda daraja na zitaonekana EPL msimu ujao.

 

Mwisho wa ligi hiyo unatoa nafasi kwa mechi za mchujo tena kupata wa kuungana na timu mbili zilizopita. Timu zitakazocheza mtoano ni Norwich, Middlesbrough, Brentford na Ipswich.

 

Timu zilizoshuka kutoka daraja hilo kwenda chini zaidi ni pamoja na zilizopata kucheza EPL, Wigan na Blackpool pamoja na Milwall.

 

Comments