Arsenal wapaa

Arsenal wapaa

 

Arsenal wamepata ushindi wao wa nane mfululizo katika Ligi Kuu ya England (EPL) na kushikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

 

Washika Bunduki wa London wakicheza ugenni kwa Burnley walifanikiwa kushinda 1-0 kwa bao la kiungo wao, Aaron Ramsey.

 

Burnley wana wakati mgumu kwa sababu wanabaki nafasi ya pili kutoka mkiani huku Arsenal wakiwa nafasi ya pili kwa pointi 66 dhidi ya 70 za Chelsea wanaongoza licha ya vijana wa Jose Mourinho kuwa na mechi mbili mkononi.

 

Katika mechi nyingine Totenham Hotspur wakicheza nyumbani walipotezewa na Aston Villa kwa kufunga 1-0, ambapo kocha wa Villa ndiye aliyefukuzwa kazi Spurs kwa madai hana ufanisi.

 

Swansea walikwenda sare ya 1-1 na Everton, Southampton wakawazidi Hull nguvu kwa 2-0, Sunderland wakapata zahama ya kupigwa 4-1 na Crystal Palace, West Bromwich Albion wakapoteza kwa Licester kwa 3-2, huku West Ham wakitoshana nguvu 1-1 na Stoke.

 

Leo mtoto hatumwi dukani, kwa sababu Manchester United wanawaalika watani wao wa jadi jijini hapo, Manchester City katika mechi ya kukata na shoka huku Chelsea wakicheza na timu dhaifu ya QPR.

Comments