NI TETESI ZA USAJILI

TETESI ZA USAJILI

 

Man City kuwabomoa Liverpool?

 

Mabingwa watetezi wa England, Manchester City wanataka kusajili wachezaji watatu kutoka Liverpool.

 

Matajiri hao wanataka kumsajili kiungo mchezeshaji, Philippe Coutinho (22),mshambuliaji Raheem Sterling (20) aliyekataa mkataba mpya Anfield na kiungo Jordan Henderson (24) anayesuasua kupokea dili jipya hapo.

 

Pamoja na kwamba Liverpool wangependa kubakiza wachezaji hao wote, wanakosa nguvu ya fedha kuchuana na klabu nyingine kubwa za England.

Jack

 

Chelsea, Manchester United na Arsenal wanawafuatilia kwa karibu beki wa kulia wa Southampton, Nathaniel Clyne (24) na kiungo wao, Morgan Schneiderlin (25).

 

Mlinzi wa Valencia, Andres Gomes (21) amekanusha madai kwamba anakaribia kujiunga na Chelsea.

 

Kwingineko, Barcelona wamesema milango ipo wazi kwa ajili ya kujadiliana na kiungo wao mkongwe, Xavi ilia pate mkataba mpya, lakini Xavi (35) anadaiwa amepanga kujiunga na klabu ya Al Sadd ya Qatar.

 

Kocha anayewasaidia Sunderland kuepuka kushuka daraja, Dick Advocaat atapewa mkataba wa mwaka mmoja iwapo atafanikisha kazi hiyo.

 

Comments