Ni Arsenal, Man U robo fainali

Mabinwga watetezi wa Kombe la FA, Arsenal watasafiri kuwavaa Manchester United katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

United wamekata tiketi yao Jumatatu baada ya kuwafunga Preston North End 3-1. Robo fainali itafanyika kati ya Machi 7 na 8.
Katika droo iliyotolewa, Liverpool watawakaribisha Blackburn huku Bradford City wakicheza na Reading.

Mahasimu Aston Villa na West Bromwich Albion watakabiliana kwenye dimba la Villa Park. Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amesema anafurahi kupangwa na Arsenal.
“Itakuwa mechi nzuri, mechi kubwa. Kucheza dhidi ya Arsenal siku zote ni mechi kubwa,” kocha huyo alisema.

Arsenal na United walikutana kwenye fainali za FA msimu wa 2004/5 FA katika uwanja wa Cardiff, ambapo Washika Bunduki wa London walishinda kwa penati 5-4 baada ya kwenda suluhu kwenye muda wa kawaida.

Comments