KAGERA SUGAR KUHAMA UWANJA

Timu ya Kagera Sugar ambayo inashiriki ligi Kuu ya Vodacom imeamua kuhama Uwanja wa CCM Kirumba uliopo Mwanza na timu hiyo itahamia Uwanja wa Kambarage Uliopo shinyanga.

kocha Msaidizi wa Kagera sugar Mrage Kabange alisema watahama Uwanja wa CCM Kirumba na Mechi zake zote za raundi ya pili zitachezwa Uwanja wa Kambarage ulipo shinyanga.

“Uwanja wa CCM Kirumba umetukataa Kabisa na Hatuna Bahati Nao tumecheza mechi 3 na zote tumepoteza” Kabange alisema
Kagera ilicheza na Azam ikafungwa 3-1,Mbeya city Ilimpiga Kagera1-0,Ndanda Imemfunga Kagera 2-1.Mechi zote zilichezwa CCM KIrumba.

Kocha Mkuu wa Kagera sugar Jackson Mayanja Ameenda Kusoma Mafunzo ya ukocha ya juu mjini Kampala,Uganda na atarudi Nchini Tarehe 5 feb.

Licha ya Uwanja pia Kagera sugar inakabiliwa na tatizo la Majeruhi kwa wachezaji wake ambao ni Benjamin Askwire,Malegesi Mwanga,Dickson Mbada,Yusuph Komba na Salum Kanoni.
Pia Kagera Sugar Haipati Mashabiki wengi Kwakuwa Inachukiwa na Watu wa Mwanza kwakuwa Kagera sugar ndio iliyosababisha Toto African ya Mwanza Kushuka Daraja.

Kagera sugar hapo awali ilikuwa ikicheza Mechi zake katika Uwanja wake wa Nyumbani wa kaitaba.Mpaka sasa uwanja wa kaitaba upo katika Matengenezo ya kuweka Nyasi bandia.

Comments