Majanga Arsenal

Arsenal wamepoteza mechi nyingine kwa kufungwa na Stoke 3-2 katika mechi iliyoanza vibaya kwao, kwani hadi nusu ya kwanza walikuwa chini kwa mabao 3-0.
Wakicheza ugenini, Arsenal walikuwa kama wameloa hadi nusu ya kwanza na walipata pigo zaidi baadaye kwa beki wao chipukizi Calum Chambers kupewa kadi nyekundu. Mabao ya wenyeji yalifungwa na Peter Crouch sekunde ya 19 tu, Bojan akatia la pili na Jon Walters akawaliza kwa la tatu.

Arsenal walirudi vyema kipindi cha pili lakini jitihada zao hazikutosha, kwani walipata mabao mawili kupitia kwa Santi Cazorla na Aaron Ramsey. Dakika 45 za kwanza zilikuwa mbaya zaidi kwa Kocha Arsenal Wenger.

Kwenye mechi nyingine Manchester City walifanikiwa kupata ushindi mwembamba dhidi ya Everton na kupunguza pengo kwa vinara wa ligi, Chelsea, kwa pointi tatu, ambapo bao la City lilifungwa na Yaya Toure kwa penati.

Matokeo mengine ni kwamba Hull walikwenda suluhu na West Bromwich Albion kama ilivyokuwa kwa Liverpool na Sunderland na Tottenham Hotspur na Crystal Palace huku Queen Park Rangers waliwalaza vibonde wenzao Burnley 2-0.

Comments