Kimetto rekodi mpya Marathon

Raia wa Kenya, Dennis Kimetto amevunja rekodi ya mbio za Marthon jijini Berlin, Ujerumani.

Kimetto (29) ameibuka mshindi kwa kukimbia kwa muda wa saa mbili, dakika mbili na sekunde 57, akivunja rekodi ya awali iliyokuwa ikishikiliwa na Mkenya mwenzake, Wilson Kipsang, aliyetumia muda wa 2:03:23 mwaka mmoja uliopita.

Mpinzani wake kwenye mbio hizo za Berlin, naye Mkenya, Emmanuel Mutai alikimbia kwa 2:03:13.

Kimetto alisema kwamba anajihisi furaha na fahari kubwa kwa kushinda mashindano hayo yaliyokuwa magumu na kwamba alikuwa vizuri tangu mwanzo, akidhamiria kuvunja rekodi ya dunia.

Kimetto amesema kadiri miaka inavyokwenda rekodi zinazidi kuvunjwa, akasema labda wakati ujao atatumia saa mbili na dakika moja tu.

Comments