Man U wakwama Sunderland

Manchester United wameshindwa kutoka kwenye mtanziko wa kuanza vibaya ligi kuu.

Vijana wa Louis van Gaal wameambulia sare ya 1-1 nyumbani kwa Sunderland, na kumfanya Mdachi huyo aendelee kusubiri ushindi wake wa kwanza.

Juan Mata alitoa matumaini kwa kufunga bao dakika ya 17 lakini likafutwa na Jack Rodwell dakika 15 kabla ya mapumziko. Kadiri muda ulivyokwenda ufanisi wa Mata kwenye wingi ulipungua kwa kuzidiwa maarifa na Lee Cattermore na pia Nahodha Wayne Rooney hakufurukuta.                           

Mbaya zaidi, Ashley Young akishambulia ndani ya eneo la penati alijirusha, wakadai penati lakini akaishia kupewa kadi ya njano.  

Van Gaal na msaidizi wake, Ryan Giggs walizama katika majadiliano kuubadili mchezo ila itabidi waridhike na pointi moja waliyopata kwani walikuwa kikawaida sana.  Itabidi Man u wajitahidi kusajili wachezaji wengine wazuri.

Comments