Man U na ‘mechi ya watoto’

LUKE SHAW NJE WIKI NNE

Maafa yaliyowapata Manchester United msimu uliopita yameanikwa wazi, ambapo kwa mara ya kwanza tangu miaka 19 iliyopita, timu hiyo inaanzia hatua ya pili kwenye michuano ya Kombe la Ligi.

Katika michuano hiyo inayodhaminiwa na Capital One, ikienda kwa jina la Capital One Cup ambayo mabingwa wa mwaka jana ni Manchester City, United wamepangwa kucheza na Milton Keynes Dons, maarufu kama MK Dons.

Mara ya mwisho kuanza kwenye hatua hii ya awali ilikuwa Septemba 1995 ambapo Manchester United walikandikwa 4-3 na York.  Timu nyingine zinazoshiriki katika hatua hii ni pamoja na Bradford, Leeds, Newcastle, Gillingham, Stoke na Portsmouth.

Mechi za hatua hiyo zimepangwa kuchezwa wiki inayoanza Aprili 24.
 
LUKE SHAW NJE WIKI NNE
shaw

Beki mpya wa Manchester United, Luke Shaw ameumia nyama za paja na atakuwa nje kwa mwezi mmoja. Shaw alisajiliwa kutoka Southampton kwa pauni milioni 27 msimu huu, na ndiye tegemeo kubwa kwenye ulinzi wa kushoto.

Hata hivyo, kocha Louis van Gaal alipoingia na kumwona kwenye mechi alisema hayupo fiti, hivyo akawekwa chini ya programu maalumu ya kumrejesha kwenye hali nzuri, lakini sasa ameumia na hataanza mechi kama tatu au nne za Ligi Kuu ya England inayoanza Jumamosi hii.

Comments