Patrice Evra ajiunga Juventus

 

Nahodha Msaidizi wa Manchester United, Patrice Evra ameamua kuachana na timu hiyo na kujiunga na Juventus ya Italia.

Evra (33) ambaye ni beki wa kushoto aliyesaini mkataba mpya na Old Trafford majuzi, ameamua kujiunga na mabingwa hao wa Italia na atashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya, kwani Man U hawashiriki chochote nje ya England msimu huu.

Mchezaji huyo anaondoka huku United wakiwa wameshamsajili beki chipukizi Luke Shaw kutoka Southampton kwa thamani ya pauni milioni 30.

Evra alikuwa mmoja wa wachezaji waliotishiwa kupigwa panga United lakini Ryan Giggs alipendekeza kwamba abaki pamoja na Rio Ferdinand. Hata hivyo mkataba wa Ferdinand haukuhuisha isipokuwa wa Evra tu.

Comments