UJERUMANI NI BINGWA, LABDA ITOKEE MIUJIZA KWA ARGENTINA

Kilele cha fainali za Kombe la Dunia kinatarajiwa kufika leo Julai 13 kwa kuzikutanisha mataifa ya Ujerumani dhidi ya Argentina. Baadhi ya mashabiki wa soka wanasema fainali ya leo ni kati ya Papa Francis (Argentina) dhidi ya Papa Benedict XVI (Ujerumani).

Pambano la Argentina na Ujerumani litaikumbusha dunia katika fainali za mwaka 1986 ambapo Diego Maradona akiwa na kikosi chao maarufu kama Albeceleste walishinda mabao 3-2 dhidi ya iliyokuwa Ujerumani Magharibi ambayo sasa ni taifa moja, Ujerumani.

Nchi hizo zimewahi kukutana mara tatu katika mchezo wa fainali wa Kombe la Dunia. Argetina iliifunga Ujerumani mwaka 1986 na kutwaa kombe hilo.

Mara ya pili kukutana katika mchezo wa fainali wa Kombe la Dunia ulikuwa mwaka 1990, ambapo Ujerumani ilishinda mchezo huo na kutawazwa mabingwa wa dunia.

Argetina ilifuzu kutokana na uzembe wa kocha Louis van Gaal ambaye aliwataka wachezaji wake sita kucheza nafasi ya ulinzi, kisha akapanga viungo watatu na mshambuliaji mmoja.

Kwanini Ujerumani inaweza kuwa bingwa? Ukiangalia muundo wa uchezaji wa timu hizi mbili zote zinacheza kwa mbinu za hali juu. Tofauti kubwa iliyo ni kwmaba Argetina wanatumia mbinu zao polepole mno. Wanapokuwa eneo la 18 la adui ndipo huanza kucheza wka kasi, na mara nyingi hutegemea ‘one-two’ na kucheza kwa nafasi.

Ujerumani wao wanaanza mashambulizi katikati ya uwanja. Wanaweza kutumia upande wa kulia, katikati ya dimba, na kushoto. Ujerumani wanaweza kutumia mashambulizi ya kushtukiza, na kuifanya ngome ya Argentina kuwa katika wakati mgumu.

Uwezo wa kucheza kwa kasi muda wote wa mchezo walionao Toni Kroos, Bastian Schweinsteiger na Sami Khedira ni silaha kubwa kwao na hatari kwa Argetina.

Ujerumani wanao washambuliaji wenye uwezo mkubwa kufunga mabao ndani ya Boksi. Wakati mabao ya nje ya Boksi yanategemea uhodari wa Toni Kroos, Khedira na Schweinsteiger.

Ujerumani pia ni hatari kwenye mipira ya kona na faulo, kwamba wanaweza kulazimisha mabao ya namna hiyo wakati wowote wa mchezo. Uzuri mwingine ni kwamba wanacheza kitimu zaidi.

Tatizo lao kubwa linaweza kuwa uwoga wa kocha Joachim Loew ambaye mare kadhaa amekuwa akibadilisha mbinu kwa kuwahofia wapinzani ambao hawapaswi kuhofiwa. Mifano yake ni mechi dhidi ya Ufaransa, ambapo aliirudisha nyuma mno timu yake badala ya kushambulia wakati wote.

Argetina wao wanaweza kucheza kwa staili ileile ya taratibu na hesabu za kiwango cha juu. Tatizo lao ni kuchelewesha mashambulizi pamoja na uhaba wa viungo wenye kushambulia wakati wote.
Javier Mascherano ni kiungo mzuri, lakini hataweza kumudu kasi ya Wajerumani endapo Lucas Biglia atakuwa akicheza taratibu mno.
Natarajia kuona Ujerumani ikiwa bingwa mpya wa Kombe la dunia, lakini wanahitaji kufanya kazi ya ziada, hawatashinda kirahisi ingawa inawezekana. Ni ujerumani tu, labda itokee miujiza.

Comments