Rudisha ashinda mbio Uingereza

Mkenya David Rudisha amerejea katika makali yake kwa kutwaa ubingwa katika mbio za mita 800 za Diamond League jijini Glasgow, Scotland.
Hii ni mara ya kwanza kwa raia huyu wa Afrika Mashariki kupata ushindi katika ardhi ya Uingereza tangu alipopata medali ya dhahabu kwenye mbio za London 2012.

Rudisha (25) alikuwa nje kidogo kutokana na majeraha lakini sasa ameweka rekodi ya dunia kwa kuwatangulia wenzake kwa dakika nzima, akikimbia dakika 1:43.34.

“Najihisi mwenye furaha kubwa sana kwa sababu nipo vizuri sasa baada ya kuwa na mwaka mgumu lakini sasa nimejiweka sawa ndio maana nilikimbia kwa kasi kubwa,” anasema Rudisha ambaye atakuwa tena Hampden Park kwa ajili ya michuano ya Jumuiya ya Madola baadaye mwezi huu.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Andre Olivier wa Afrika Kusini huku mshindi wa medali ya dhahabu wa Marekani, Allyson Felix na Mjamaica Shelly-Ann Fraser-Pryce walifuatia, nao wakiwa pia wanatoka kwenye majeraha.

Posted under:  All Articles, Athletics, Sport, Sports, Sports News

Tags:  ,

Comments