Di Stefano shujaa wa soka afariki

ASHLEY COLE ASAJILIWA ROMA

Shujaa wa kimataifa wa soka, Alfredo Di Stefano aliyewika  Real Madridameaga dunia akiwa na umri wa miaka 88.

Huyu ni mtu ambaye anachukuliwa kuwa mchezaji bora zaidi katika historia ya soka, na ameondoka duniani wakati fainali za Kombe la Dunia zikiendelea.

Di Stefano aliyepata kuwa rais wa heshima klabuni hapo alikuwa hajitambui kwa muda katika hospitali moja jijini Madrid.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Madridi alifunga mabao katika fainali za 1956 na 1960. Mkongwe wa England, Sir Bobby Charlton aliyecheza na Di Stefano amemwelezea kuwa mmoja wa wacheazji bora kabisa aliopata kuwaona.

“Ulimwengu wa soka umepoteza mchezaji bora kabisa, mtu wa aina yake … nina kumbukumbu nzuri sana za enzi zangu naye, nimepata heshima kubwa kumuita rafiki yangu,” akasema Charlton ambaye ni mmoja wa wakurugenzi katika klabu ya Manchester United.

Anasema kwamba Di Stefano alikuw na uwezo wa kukaba, kugawa mipira na hata kushambulia na akiwa kwenye mechi ilikuwa burudani kwa watazamaji lakini kilio kwa adui zake katika timu pinzani

ASHLEY COLE ASAJILIWA ROMA
Zemanta Related Posts Thumbnail

Klabu ya Roma ya Italia imemsajili beki wa zamani wa kushoto wa Chelsea, Ashley Cole kwa mkataba wa miaka miwili.

Cole (33) amejiunga na klabu hiyo ya ligi kuu ya Italia akiwa mchezaji huru baada ya Jose Mourinho kumtupia virago Stamford Nridge.

Roma wametuma salamu za kumkaribisha beki wao huyo mpya kwenye mtandao wa Twitter akiondoka England ambako mbali na kutemwa na Chelsea aliachwa pia na timu ya ta

Comments