Uholanzi robo fainali

 *Costa Rica wawazamisha Ugiriki

Klaas Jan Huntelaar amefunga bao la penati katika dakika za mwisho za mechi dhidi ya Mexico na kutinga robo fainali.

Uholanzi walitoka nyuma wakiwa wametangulia kufungwa 1-0 hadi kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 katika hali iliyowahuzunisha sana Mexico.

 

Bao la Mexico lilifungwa na Giovani dos Santos na bao hilo likasimama na kuwapa kila aina ya matumaini washabiki kwamba wangefuzu.

Hadi dakika mbili kabla ya muda wa ziada, Wadachi walikuwa wameshalala kwa bao hilo moja ambalo lilisawzishwa na Wesley Sneijder.

 

Wakati ikidhaniwa mambo yangemalizika kwa 1-1 na hivyo kulazimika kwenda katika muda wa ziada, mkongwe Arjen Robben alichezewa rafu na Rafael Marquez hivyo kutolewa adhabu ya penati.

Jukumu hilo alibebeshwa mchezaji Huntelaar aliyeingia dakika ya 76 kuchukua nafasi ya Roben van Persie.

 

Huntelaar ambaye alikosa mkwaju wake uliopita wa penati alipewa jukumu hilo na kocha ajaye wa Manchester United, Louis van Gaal na hakumwangusha.

Costa Rica wawazamisha Ugiriki
20140625-093705-34625288.jpg
Costa Rica wamewatoa Ugiriki katika mechi ngumu ambayo walicheza wakiwa watu 10 kwa zaidi ya saa moja.
Wachezaji hao wa Amerika ya Kati walipata ushindi kwa penati 5-3 baada ya kwenda sare ya 1-1 katika muda wa kawaida.
Ugiriki walichomoa bao dakika za majeruhi kupitia kwa Sokratis Papastathopoulos wakisawazisha bao la mchezaji wa Fulham, Bryan Ruiz. Dakika 30 za nyongeza hazikutoa mshindi.
Costa Rica walijituma ipasavyo licha ya upungufu wa idadi na walitulia vyema wakati wa kupiga penati, wakatumbukiza zote kimiani na sasa watacheza na Uholanzi Jumamosi katika hatua ya robo fainali.
Costa Rica walikuwa wakipewa nafasi ya mwisho katika kundi lao ambapo timu nyingine zilikuwa England, Italia na Uruguay.

Comments