Manchester United wamnasa Shaw

Manchester United wamemsajili beki wa kushoto wa Southampton na Timu ya Taifa ya England, Luke Shaw
United wanaelezwa kwamba wamemsajili mlinzi huyo kwa kitita cha pauni milioni 27, ikiwa ni baada ya Mwingereza huyo kuwaambia Saints juu ya tamaa yake ya kuchezea Man U.
Shaw (19) ni mchezaji mzuri na malipo ya dili lake yanasemwa yanaweza kuongezeka hadi pauni milioni 31 kutegemeana na ufaisi wake dimbani. Mei mwaka huu Saints walikataa dau la awali la pauni milioni 27 wakisema kwamba beki huyo alikuwa hauzwi.
Shaw amesainiwa kwa mkataba wa miaka minne ambapo kuna kipengele cha kuweza kuuongeza kwa mwaka mmoja zaidi.
Mwenyewe Shaw amesema kwamba anataka kujiendeleza kisoka akiwa na Man United kwa sababu anaamini ndiyo sehemu mwafaka kwake kuwa na kutekeleza ndoto hiyo.
Kocha Msaidizi wa Man U, Ryan Giggs amesema kwamba Shaw ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu na anatarajiwa kufanya makubwa katika siku zijazo kwenye ulimwengu wa soka.
Huyu ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Man U baada ya Ander Herrera (24), Mhispania aliyechukuliwa kutoka Athletic Bilbao kwa ada inayokadiriwa kuwa pauni milioni 29.
Wayne Rooney alikuwa mchezaji mdogo zaidi kusajiliwa Old Trafford 2004 kwa pauni milioni 20, kwa hiyo usajili wa Shaw unampiga kumbo na unaendana na ule wa Marquihos aliyesajiliwa Paris St-Germain kutoka Roma Julai.

Comments