Nigeria wafuzu kwa mtoano

Nigeria wamekuwa taifa la kwanza Afrika kufuzu katika hatua ya makundi katika fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka huu.

Nigeria wamefanikiwa kusonga mbele baada ya kutia kibindoni pointi nne kwa kushinda mechi moja, kwenda sare moja na kufungwa moja.

 

Walikuwa wakiwania nafasi ya pili nyuma ya Argentina na Iran ambao walikuwa na pointi moja.

Nigeria walifungwa na Argentina 3-2 Jumatano hii ambapo mabao mawili ya Argentina yalifungwa na Lionel Messi huku Ahmed Musa wa Nigeria akisawazisha moja baada ya jingine.

Lile la tatu na la ushindi kwa Argentina lilifungwa na mchezaji Rojo.

 

Stephen Keshi anakuwa kocha wa kwanza Mwafrika kuwavusha Waafrika hadi hatua ya mtoano, kwani timu nyingine zilizofuzu zimekuwa zikifundishwa na Wazungu, Wamarekani au Waasia.

Iran waliangukia pua baada ya kufungwa na Bosnia-Hercegovina katika mechi yao ya mwisho. Nigeria waliwafunga Bosnia na kwenda suluhu na Iran katika mechi zake za awali.

 

Argentina wameshinda mechi zao zote tatu na katika hatua ya mtoano Nigeria watachuana na Ufaransa ambao wameshinda mechi mbili na kwenda sare moja.

Comments