Real Madrid wamkamia Suarez

*Kuwapa Liverpool £30m na Morata

Real Madrid wamezidisha shinikizo kwa Liverpool wakitaka kumsajili mpachika mabao wao namba moja, Luis Suarez.

Safari hii Real wameweka mezani dau la pauni milioni 30 na wamewaahidi kuwapa mshambuliaji mmoja juu yake.

Ofa hiyo inakuja baada ya Suarez kung’ara kwenye mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya England ambapo alifunga mabao yote mawili ya timu yake ya Uruguay.

Rais wa Bernabeu, Florentino Perez anayejulikana kwa kuongoza kwa kununua wachezaji ghali zaidi duniani, amedhamiria kumpata Suarez ili Real wawe wakali zaidi msimu ujao.

Pamoja na pauni hizo milioni 30, Real wanamtoa na mshambuliaji wao kinda Alvaro Morata aende Anfield.

Itakuwa ngumu, hata hivyo, kwa kocha Brendan Rodgers kukubali dili hilo maana msimu uliopita aliwakatia Arsenal walipotoa pauni 40,000,001 ambazo zilifikia kigezo cha kifungu cha mkataba wa Suarez.

Haijatambulika hata hivyo iwapo kwenye mkataba wake mpya kuna kifungu chochote kinachomwezesha kuondka iwapo timu itafikia dau fulani.

Morata ni mchezaji mzuri na anawania na klabu mbalimbali ndani nan je ya Hispania.

Comments