Costa Rica wawatungua Uruguay

 

Costa Rica wamewaadhiri Uruguay kwa kuwatungua mabao 3-1.

Katika mechi hiyo ambayo Uruguay walimpumzisha mshambuliaji machachari wa Liverpool, Luis Suarez, Uruguay walianza kupata bao kwa penati iliyopigwa na Edinson Cavani katika dakika ya 24.
Hata hivyo, mechi hiyo ya Kundi D walimo England na Italia ilibadilika kwa mshambuliaji wa Arsenal,
Joel Campbell kusawazisha katika dakika ya 54. Campbell anacheza kwa mkopo Olympiakos.

Dakika tatu baadaye, Costa Rica walipiga bao la pili kupitia kwa mlinzi wake, Oscar Duarte na kuwasisimua washabiki wao.
Kana kwamba hiyo haitoshi, akitokea benchi, Marcos Urena alinasa mpira wa Campbell na kumtungua kipa wa Uruguay, Fernando Muslera.

Mambo yalizidi kuwa mabaya kwa Uruguay kwa mchezaji wao, Maximiliano Pereira kupewa kadi nyekundu katika muda wa ziada kwa rafu isiyokuwa na lazima dhidi ya Campbell na sasa atakosa mechi ya Alhamisi dhidi ya England.

Comments