Carlos Vela anarudi Arsenal

Arsenal wameamua kumrejesha kundini mchezaji wake wa zamani, Carlos Vela.

Mshambuliaji huyo alikuwa katika timu ya Real Sociedad kwa misimu minne lakini sasa Arsenal wameamua kutumia kifungu cha mkataba ambapo watampata kwa pauni milioni 3.5 tu.

Mshambuliaji huyo raia wa Mexico atakuwa Emirates msimu ujao licha ya jitihada za Rais wa Sociedad, Jokin Aperribay kutua London kuwashawishi Arsenal wamwache akae Hispania.

Vela (25) alisajiliwa na Arsenal Januari 2006 lakini hakung’ara sana kabla ya kupelekwa kwa mkopo Salamanca na Osasuna kisha akarudi Arsenal 2008.

Alipelekwa tena West Bromwich Albion kisha Sociedad, kabla ya kusajiliwa rasmi huko 2011. Akiwa Arsenal alifunga mabao 11 katika miaka sita, lakini amekuwa juu nchini Hispania msimu uliopita ambapo alifunga mabao 16 katika mechi 34.

Comments