Arsenal mabingwa FA

 
Hatimaye Arsenal wamemaliza kiu ya taji baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la FA.
Aaron Ramsey ambaye alikuwa tegemeo kubwa kwenye msimu katika ligi kuu ndiye aliwang’arisha Arsenal kwa bao la dakika ya 109.

Arsenal waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo walikjikuta wakiachwa nyuma kwa kufungwa mabao mapema dakika ya nne na ya nane kabla ya kukomboa dakika za 17 na 71.

Ilikuwa shamrashamra ya aina yake kwenye Uwanja wa Wembley na miaka tisa iliyopita Arsenal walitwaa kombe hili mikononi mwa Manchester United katika Uwanja wa Cardiff.

Wenger sasa anaweza kuanza maandalizi ya msimu mpya ujao vizuri kwa kuwa na kikombe, maana alishasema kuwa hata angekikosa angebaki kuwa kocha wa Washika Bunduki wa London.
 

Comments