Man City mkao wa kula

Timu ya Manchester City imepalilia vyema safari ya kutwaa ubingwa kwa mara ya pili katika miaka mitatu.

City walibanwa nyumbani kwao na Aston Villa kwa zaidi ya saa nzima, kabla ya Edin Dzeko kuwafyatua kwa mabao mawili ya haraka.

Kocha Manuel Pellegrini alijitahidi kuelekeza vijana wake, huku Paul Lambert upande wa pili akiwachagiza wake, waliofanikiwa kuwa na ngome kali hadi kipindi cha pili katikati.

Bao la Steven Jovetic na Yaya Toure dakika za mwisho yaliwazamisha Villa na kufanya Etihad ilipuke kwa vifijo na hoi hoi.

Ushindi huo umeipandisha City kileleni, wakiwazidi Liverpool kwa pointi mbili na idadi kubwa ya mabao ya kufunga kabla ya mechi za mwisho wikiendi hii.

Comments