Mourinho amtishia Hazard

*Guardiola hajui hatima yake

Matokeo mabaya kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) yamewachanganya makocha wa Chelsea na Bayern Munich.

Wakati Jose Mourinho wa Chelsea akimalizia hasira zake kwa mchezaji kinda na mahiri, Eden Hazard kwa kumchagiza, Pep Guardiola amesema kwamba Bayern wanatakiwa kutafakari iwapo yeye ndiye anafaa kuwa kocha wao.

Hazard alimbwatukia kocha wake kwa mbinu zake na sasa Mourinho amemtishia huku akisema kwamba winga huyo bado hajaanza kujituma kabisa kwa ajili ya klabu yake.

Inaelezwa kwamba Paris Saint-Germain wa Ufaransa wanamwania Hazard kwa ajili ya msimu ujao na ndiye amekuwa nguzo muhimu kwa Chelsea lakini timu hiyo ya London ilifungwa 3-1 na Atletico Madrid Uwanja wa Stamford Bridge na kuwachukiza washabiki wa Chelsea.

Mourinho anasema kwamba Hazard alifanya makosa kwenye mechi hiyo na kuruhusu bao la kwanza na kusema ni aina ya wachezajiw asiotoa suluhu ya tatizo bali wanalaumu tu.

Katika hatua nyingine, Guardiola amesema kwamba ni juu ya Bayern kuamua hatima yake. Bayern walifungwa 4-0 na Real Madrid.

Comments