Kwa heri Tito Vilanova

Kocha wa aliyejiuzulu Barcelona, Tito Vilanova (45) amefarki kwa saratani ya koo.

Alijiusulu ukocha Barca Julai mwaka jana ili aendelee na matibabu yake na mikoba kuchukuliwa na Gerardo Martino.

Vilanova alikuwa na uvimbe katika koo lake na uliondolewa Novemba 2011, lakini mwaka jana alipata matatizo zaidi yanayohusiana na ugonjwa huo.

Vilanova alikuwa msaidizi wa Joseph ‘Pep’ Guardiola ambaye zaidi ya mwaka mmoja uliopita aliachia ngazi akisema anahitaji kupumzika na kuona akili yake upya, ambapo sasa amejiunga na mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich.

Kocha huyo alianzia kwenye timu ya vijana ya Barca 1988, kabla ya kujiunga na Celta Vigo na baadaye na klabu nyingine.

Amepata kuwa mkurugenzi wa ufundi kwenye klabu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Terrassa, na baadaye kuwa kocha msaidizi wa timu ya pili ya Barca, akifanya kazi chini ya Guardiola, kabla ya 2008 kuwa msaidizi wa kocha huyo.

Vilanova alikaa New York, Marekani kwa wiki 10 kwa ajili ya matibabu yake hayo na alirejea Hispania Machi, ambapo aliiongoza klabu yake kutwaa ubingwa wa nchi hiyo.

Rais wa Barca, Sandro Rosell na mkurugenzi wa soka, Andoni Zubizarreta ndio waliotangaza habari hizo mbele ya waandishi wa habari, wakisema Vilanova anaendelea na matibabu, hivyo hataweza kuendelea na majukumu hayo, wakisema ni pigo kubwa kwa klabu.

Klabu hiyo imekuwa na Jordi Roura kama kaimu kocha wakati Vilanova akiwa kwenye matibabu na mapumziko. Apumzike kwa amani.

Posted under:  All Articles, Featured, Sport, Sports, Sports News

Tags:  , , ,

Comments