Chelsea wawazuia Atletico Madrid

Chelsea wamecheza kwa kujihami na kufanikiwa kutoka suluhu ugenini jijini Madrid dhidi ya Atletco Madrid katika mechi ya nusu fainali Ligi ya Bingwa Ulaya.

Katika mechi hiyo ya kwanza Chelsea walitumia kila mbinu kuzuia wapinzani wao ambao ni wakali hivyo uamuzi wa kuingia fainali utaamuliwa kwenye mechi ya marudiano jijini London.

Chelsea wameondoka huko na majeruhi wawili, kipa Petr Cech aliyeumia bega hivyo nafasi yake hadi mwisho wa msimu inatarajiwa kushikwa na mkongwe Mark Schwarzer. John Terry naye aliumia na atakuwa nje kwa mechi zilizobaki za ligi kuu.

Kipa wa Atletico Madrid, Thibaut Courtois alionesha umahiri wa aina yake alipocheza dhidi ya klabu yake mama na nafasi pekee ambayo Chelsea walielekea wangefunga ni aliyopata Ramires lakini akapiga nje.

Comments