Liverpool wawachapa Man City

Liverpool wameonesha nia ya dhati kuutaka ubingwa wa England kwa kuwafyatua Manchster City 3-2.
Ilikuwa mechi kubwa na muhimu kwa timu zote zinazowania ubingwa, huku Liverpool wakiadhimisha miaka 25 ya mauaji ya Hillsborough.

Liverpool walionekana kuwa wazuri tangu mwanzo, ambapo mabao ya Raheem Sterling na Martin Skrtel dakika ya sita nay a 26 yaliwaweka mbele na kujiamini vijana hao wa Brendan Rodgers.

Hata hivyo katika kipindi cha pili, City ambao walimpoteza Yaya Toure aliyeumia, walirejea kwanguvu kipindi cha pili ambao David Silva alichomoa moja kisha majalo yake kumgonga Glen Johnson na kipa Simon Mignolet kabla ya kujaa wavuni na kusawazisha mambo.

Dakika 12 kabla ya mchezo kumalizika, Nahodha wa Man City, Vincent Kompany alikosea kuokoa na kumpa mpira Philippe Coutinho wa Liverpool aliyeukwamisha wavuni baada ya kipa Joe Hart kuukosa.
Katika mechi nyingine, Chelsea waliwafunga Swansea 1-0, kufikisha pointi 75 hivyo kuwa nyuma ya Liverpool kwa pointi mbili.

Man City wamebaki na pointi zao 70 katika nafasi ya tatu wakati Everton wana pointi 66 na Arsenal 64. Hata hivyo Man City wana mechi mbili mkononi na wakishinda zote watakuwa juu.

Comments