La Liga ya farasi watatu

*Atletico wawazidi Barca, Real

Atletico Madrid, Barcelona na Real Madrid zimepata pointi tatu kila moja kwenye mzunguko wa 31 wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga.

Wakati Real Madrid wanaoshika nafasi ya tatu waligawa kichapo cha haja ; mabao 5-0 dhidi ya Rayo Valecano, Lionel Messi alifunga bao la penati  kwa Barcelona waliocheza na Espanyol na kuondoka na ushindi huo mwembamba.

Mabao ya Real Madrid yalifungwa na Gareth Bale mawili; nyota wao, Cristiano Ronaldo, beki wa kulia Dani Carvajal na Alvaro Morata anayewaniwa na baadhi ya timu za Ligi Kuu ya England.

Bale amefikisha mabao 12 katika ligi na pia ametoa pasi 12 zilzozaa mabao idadi hiyo hiyo wakati kwenye mashindano yote kwa ujumla amefunga mabao 15 katika mechi 34. Katika mechi za mwanzo alikuwa ama akiugua au kutozoea mazingira mapya baada ya kusajiliwa kutoka Tottenham Hotspur kwa dau kubwa na kuwa mchezaji ghali zaidi.

Vinara wa ligi, Atletico nao walipata pointi tatu muhimu kubaki kileleni, walipowafunga Athletic Bilbao 2-1, mabao yao yakifungwa na Diego Costa na Koke. Atletico wamefikisha pointi 76, Barca 75 na Real 73. Nafasi ya nne inashikwa na Bilbao wenye pointi 56 na hawahesabiwi katika mbio za ubingwa.

Comments