Chelsea watinga robo fainali Ulaya

*Real Madrid nao wapita

Chelsea wamefanikiwa kuingia robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) baada ya kuwapiga Galatasaray 2-0 kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Mabao ya Samuel Eto’o na Garry Cahil yalitosha kuwazamisha vijana wa Roberto Mancini ambao katika mechi ya awali walitoka sare ya 1-1.

Galatasaray walicheza hovyo licha ya kuwa na wachezaji mahiri kama Didier Drogba aliyepata kukipiga Chelsea na alikuwa amesema ana ndoto ya kufunga bao, huku Mancini akiota kupata mlo na Jose Mourinho baada ya kumfunga.

Chelsea wanakuwa timu ya kwanza ya England kufika hatua hiyo msimu huu, baada ya Arsenal na Manchester City kutolewa katika hatua ya 16 bora. Manchester United wanajitupa uwanjani kukipiga na Olyimpiakos wakiwa na deni la mabao mawili waliyofungwa ugenini Ugiriki.

REAL MADRID WAWATOA SCHALKE 04

Cristiano Ronaldo alifunga mabao mawili na Alvaro Morata moja katika mechi nyingine, ambapo Real Madrid waliwatoa mashindanoni Schalke 04 ya Ujerumani.

Kipigo hicho cha mabao 2-1 kinawafanya Madrid kuwatoa wapinzani wao hao kwa jumla ya mabao 9-2. Bao la Wajerumani hao lilifungwa na Tim Hoogland lakini likawa kama tone la maji baharini.

Comments