Yanga ” Waturuki” warudi kileleni VPL

Yanga “wazee wa Uturuki” leo waliweza kuibuka na ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Ashanti united watoto wa Ilala kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.Yanga ilikuwa ya kwanza kupata bao mnamo dakika ya 51 kupitia kwa mshambuliaji wake raia wa Barudi Didier Kavumbagu na baadae vijana wa kocha King Kibaden, Ashanti United walisawazisha kupitia kwa mshambuliaji wao Raia wa Nigeria Bright Obina dakika ya 60. Mnano dk ya 79, alikuwa ni David Luhende ambeya alifunga goli la pili na la ushindi kwa Yanga.

Nayo Azam Fc ilikuwa na kibarua kigumu nyumbani kwake Chamazi Complex dhidi ya Mtibwa sugar ya mjini Morogoro na mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika,Azam Fc waliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 goli lililofungwa na mshambuliaji raia wa Ivory Coast Kipre Tchetche.

Mkoani Kagera wenyeji Kagera sugar waliwakaribisha watoto wa Jiji la Mbeya,timu ya mbeya city katika dimba la kaitaba na mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, watoto wa kocha Juma Mwambusi mbeya city waliweza kuibuka na pointi zote 3 kwa ushindi wao wa bao 1-0. Shukrani kwa bao pekee lililofungwa na swita Julius.

Mkoani Tanga kulikuwa na mpambano kati ya mwenyeji Coastal union dhidi ya maafande wa Jkt Oljoro. Coastal Union walikuwa wa kwanza kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Yayo Kato lakini kutokana na kuonyesha mchezo mbovu na beki ya Coastal Union kuonyesha mapungufu mengi, mnamo dakika ya 87 ya mchezo, hamis Saleh alifanikiwa kusawazisha bao hilo. Hadi mwisho wa mchezo, Coastal Union 1-1 Jkt Oljoro.

kwa matokeo hayo,Yanga wanaendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na pointi 31 huku Azam wakibakia katika nafasi ya 2 wakiwa na pointi sawa na Mbeya city waliopo nafasi ya 3 wote wakiwa na pointi 30 na kutofautiana kwa magoli ya kufunga na kufungwa. Michezo mingine inatarajiwa kupigwa hapo kesho kwenye viwanja mbalimbali.

Comments