Chelsea, Man U watesa EPL

Chelsea wamenyakua nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi baada ya kuwanyuka Hull 2-0.

Yalikuwa mabao ya Eden Hazard na Fernando Torres yaliyowatuliza vijana wa Jose Mourinho hapo KC Stadium.

Chelsea wamepata faida ya kuongoza, pengine kwa sababu waliokuwa vinara wa ligi Arsenal na Manchester City wanacheza Jumapili na Jumatatu kwa mtiririko huo, ambapo Chelsea wamepata ushindi wa nane katika mechi 11.

Katika mechi nyingine, Manchester United walifanikiwa kupata ushindi muhimu wa mabao 2-0 dhidi ya Swansea katika dimba la Old Trafford. West Ham waliokuwa wameadhiriwa kwa kufungwa mabao 11 katika mechi mmbili tu walijiweka sawa kama kocha wao, Sam Allardyce alivyoahidi wakawafungwa Cardiff 2-0.

Kwingineko Sunderland walipata ushindi wa 4-1 dhidi ya Fulham, Southampton wakawafunga West Bromwich Albion 1-0, Everton wakawafunga Norwich 2-0 na Tottenham wakafurahia ushindi wa 2-0 dhidi ya Crystal Palace.

Kwa matokeo hayo timu zinazoongoza kuendana na namba ni Chelsea, Arsenal, Man City na Everton.
Nafasi za mwisho zinashikwa na Cardiff wenye pointi 18, Sunderland wenye pointi 17 sawa na Crystal Palace.

Comments