Manchester United nje FA Cup

Si bahati yao hadi sasa mwaka huu. Ndivyo unavyoweza kusema kwa Manchester United.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya England (EPL) wametolewa kwenye Kombe la Chama cha Soka (FA) cha England kwa kufungwa jumla ya mabao 2-1.

Wakicheza nyumbani Old Trafford, Mashetani Wekundu walitaka kutoa mkosi wa kupoteza mechi ya EPL dhidi ya Tottenham Hotspur lakini haikuwezekana.

Kocha David Moyes atakuwa amesikitika na kuchukia sana kwa sababu hii ni mara ya kwanza katika historia ya Swansea kushinda mechi katika dimba la Old Trafford, ikiwa ni muda mfupi tangu alipochukua mikoba ya Sir Alex Ferguson.

Wilfred Bony ndiye alikuwa shujaa kwa bao lake la dakika ya 90 lililowafurusha Manchester United katika Kombe la FA.

Bony, mshambuliaji wa Kidachi alikuwa amesababisha sintofahamu muda mrefu kwa ngome ya United aliunganisha majalo ya Wayne Routledge na kuwavusha kwenye hatua ya nne.

Ilishaelekea kwamba mechi ingerudiwa kutokana na kwenda sare ya 1-1 na pia mchezaji wa United, Fabio Da Silva alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 80 lakini haikudhaniwa kwamba ingewaathiri wenyeji.

Swansea waliowafunga United hawajapata kushinda katika mechi zao saba zilizopita 
Lakini walitangulia kufunga kupitia kwa Routledge kabla ya Javier Hernandez kusawazisha katika mechi iliyochezeswa na Mike Dean na kuhudhuriwa na watazamaji zaidi ya 73,000.

Katika mechi nyingine Nottingham Forest waliwachakaza West Ham 5-0, Sunderland wakawashinda Carlisle 3-1 huku Derby wakilazwa na Chelsea 2-0, Liverpool wakashinda 2-0 dhidi ya Oldham wakati Port Vale wakienda sare ya 2-2 na Plymouth.

Wote waliotoka sare au suluhu watarudiana kwenye uwanja wa mgeni wakati walioshinda wanasonga kwente awamu inayofuata na walioshindwa wametolewa.

Comments