Arsenal yauwa, Liverpool yapunguzwa kasi…

 

Liverpool leo wamejikuta wakiangukia nafasi ya nne baada ya kula kichapo cha 2-1 toka kwa Manchester city ambao wanaonekana kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza mchezo wa ligi kuu wanapokuwa uwanja wao wa nyumbani Etihad.Liverpool walipata bao kupitia kwa mbrazil Coutinho kabla ya Vincent Kompany na Alvaro Negredo kuipatia ushindi man city.

Manchester united pamoja na kumaliza mchezo wao wakiwa wachezaji 10 uwanjani kufuatia kadi nyekundu aliyopewa Antonio Valencia,walifanikiwa kushinda kwa bao 3-2.Hull city ilikuwa ya kwanza kupata mabao mawili ya awali kabla ya chris smalling na wayne Rooney kuifungia united huku Chester akijifunga goli na kuifanya man united kushinda kwa goli 3-2.

Arsenal leo imefanikiwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu baada ya kuifunga Westham united kwa mabao 3-1.Westham walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Carlton Cole huku Gunners wakipata mabao yao kupitia Theo walcott aliyefunga mabao mawili na Mjerumani Lukas Podolski akifunga bao la tatu.Ushindi huo unafanya Arsenal “The Gunners” kurudi katika uongozi wa ligi kuu Uingereza.

Chelsea “the Blues” wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Swansea city na kuendeleza rekodi ya kocha wao Jose Mourinho ya kutopoteza mchezo wowote wa ligi kuu Uingereza anapokuwa Stanfford Bridge.Goli hilo la chelsea nililtiwa wavuni na fundi wa Ubelgiji,Eden Hazard.

Everton leo hii wameweza kupoteza mchezo wao dhidi ya Sunderland,mchezo huo ambao ulikuwa na upinzani wa aina yake ambapo Sundeland walijipatia bao kupitia kwa kiungu toka korea kusini Ki Sung kwa mkwaju wa penalty na kuwaacha watoto wa Roberto Martinez wakiwa hawaamini kilichotokea.

Kufuatia matokeo haya, Arsenal wanaendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza.

Comments