Arsenal, Chelsea ngoma nzito

Mchezo ulikuwa doro..

 

Arsenal na Chelsea wamegawana pointi moja moja katika mechi muhimu na kuwaacha Liverpool kileleni.

Katika mechi hiyo ngumu katika dimba la Emirates, Arsenal walicheza vyema na kunyimwa penati baada ya Theo Walcott kuchezewa rafu.

Kadhalika Cesar Azpilicueta alifanikiwa kuokoa bao lililoelekezwa kimiani na Bacary Sagna kwa kichwa.

Kwa matokeo hayo, Arsenal wanakuwa katika nafasi ya pili nyuma ya Liverpool licha ya kuwa wamefungana kwa pointi.

Man City wapo nafasi ya tatu kwa pointi 35 wakati Chelsea na Everton wanazo 34 kila mmoja.

Mkiani mwa ligi wapo Crystal Palace na fulham wenye pointi 13 kila mmoja na Sunderland wenye pointi 10.

Comments