Majanga Tottenham Hotspur


*West Ham wawanyuka Kombe la Ligi
*Man United nao waingia nusu fainali

Maisha bado ni magumu White Hart Lane, kwani hata baada ya kumfukuza Andre Villas-Boas, Tottenham Hotspur wameendelea kuwa majangani.

Usiku wa Jumatano hii wamejikuta katika wakati mgumu, wakikumbukia kikombe cha mwisho, bila kujali kidogo namna gani, walichokipata 1980.

Spurs walitangulia kufunga bao kupitia kwa Emmanuel Adebayor aliyerejeshwa kikosini sambamba na Jermain Defoe kuwaweka pembeni ‘maswahiba’ wa AVB, lakini timu haikuweza kushikilia bao hilo la dakika ya 67.

West Ham wanaonolewa na Sam Allardyce walisawazisha bao hilo kupitia kwa Matt Jarvis kabla ya kijan Modibo Maliga kupachika bao la ushindi dakika chache tu kabla ya kipenga cha mwisho.

Wachezaji wa Spurs pamoja na mwenyekiti wao, David Levy walionekana kutoamini kilichotokea, lakini ndio hivyo, West Ham wamewang’oa kwenye michuano ya Kombe la Ligi.

Katika mechi nyingine, Manchester United waliwafunga Stoke 2-0 kwa mabao yaliyofungwa na Ashley Young na Patrice Evra, lakini mambo hayakuwa marahisi, kwani United walienda hadi kipindi cha pili.

Kutokana na matokeo hayo, nusu fainali itakuwa baina ya Manchester City na Sunderland wakati Manchester United atakabiliana na West Ham baadaye mwezi ujao wa Januari.

Comments