KOMBE LA LIGI ENGLAND, MZUNGUKO WA NNE….

Arsenal wapangwa na Chelsea
*Man United na vibonde Norwich
 
Ratiba ya mzunguko wa nne wa Kombe la Ligi la Capital One itawakutanisha Arsenal na Chelsea.

Arsenal waliovuka kwa njia ya penati mbele ya West Bromwich Albion wiki hii watakuwa wenyeji wa matajiri hao wa London.

Hata hivyo, kocha Arsene Wenger alipanga kikosi cha pili, akiwajaribu vijana wake wadogo na wakongwe waliokuwa ama nje kwa mkopo au majeraha.

Zawadi ya Manchester United baada ya kuwashinda mabingwa mara nane wa kombe hilo, Liverpool imekuwa ni kucheza na timu dhaifu ya Norwich kwenye awamu ijayo.

Newcastle wamerudishwa mdomoni mwa Manchester City ambao katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya England (EPL) walikutana na City wakashinda kwa mabao 4-0.
Birmingham City waliowavua ubingwa Swansea watakutana na Stoke.

Tottenham Hotspur  watakabiliana na Hull wakati Sunderland watavaana na Southampton ambao katika ligi kuu walikutana na kwenda sare.

 Burnley wanaotamba kwenye Ligi Daraja la Pili (Championship) watakuwa wenyeji wa West Ham huku Fulham wakifunga safari kwenda kucheza na Leicester.

Mechi hizo zitachezwa kati ya Oktona 29 na 30. Mabingwa wa msimu uliopita ambao wameshavuliwa ni Swansea; mwaka 2012 mabingwa walikuwa Liverpoo; mwaka uliotangulia walikuwa Birmingham City wakati mwaka 2009 na 2010 Manchester United walichukua kombe hilo.
 

Comments