Kicheko Chelsea, Spurs

Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya England (EPL) umeendelea kwa kicheko kwa klabu mbili za London.
Chelsea wanaotoka upande wa magharibi walifurahia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu mpya iliyopanda daraja ya Hull wakati Tottenham Hotspur wa London Kaskazini waliwashinda wageni wengine Crystal Palace kwa bao 1-0 la tuta.
Vijana wa Jose Mourinho walipata mabao yao kupitia kwa Oscar na Frank Lampard katika nusu ya kwanza ya mchezo, na kumhakikishia Mourinho marejeo mema.

20130729-213015.jpg

Lampard, hata hivyo, anayeaminika sana kwa kufunga penati, alikosa katika mkwaju wake wa kwanza msimu huu, kwani uliokolewa na kipa Allan McGregor, kabla ya Kevin de Bruyne kumtengea Oscar pande lililoleta bao.
Alikuwa McGregor tena aliyesababisha bao la pili, ambapo Lampard ambaye ni kiungo wa timu ya taifa ya England, alifunga kwa mkwaju wa adhabu ndogo.
Kipindi cha pili Hull walionekana kujitahidi kuwakabili Chelsea ili kurejesha mabao na pengine kupata ushindi, lakini hawakuwa na uwezo huo.
Mourinho akizungumzia ushindi huo, alisema kwamba alikuwa mahali pake, uwanja wake na kwa watu wake.
Kwa upande wa vijana wa Andre Villas-Boas, walipata bao lao la ushindi kwa mkwaju wa penati uliopigwa na mchezaji mpya, Roberto Soldado aliyevunja rekodi ya klabu kwa kusajiliwa kwa pauni milioni 26 kutoka Valencia ya Hispania.
Penati hiyo ilitolewa baada ya majalo ya Aaron Lennon kushikwa na beki Dean Moxey. Hata hivyo, kocha wa Crystal Palace, Ian Holloway alieleza kutoridhishwa na jinsi waamuzi walivyochezesha pambano hilo.
Spurs walicheza bila nyota wao, Gareth Bale anayetakiwa na Real Madrid, kwani inadaiwa kwamba ana majeraha ya mguu.
Inaweza kuwa mapema sana kutoa msimamo wa ligi, lakini mabingwa watetezi Manchester United wanaongoza kwa kuwa na pointi tatu, lakini wanawazidi mabao na kwa mpangilio huu washindani wao; Aston Villa, Chelsea, West Ham, Fulham, Liverpool, southampton na Spurs.

Enhanced by Zemanta

Comments