*KIKOSI CHA MOROCCO KUTUA NCHINI IJUMAA*

Timu ya Taifa ya Morocco (Lions of the Atlas) inatarajiwa kuwasili nchini
keshokutwa Ijumaa kwa ndege ya Emirates tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe
la Dunia dhidi ya Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Jumapili katika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Msafara wa timu hiyo yenye watu 58 wakiwemo maofisa 19 na waandishi wa
habari 12 utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
saa 8.55 mchana na utafikia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency.

Siku hiyo Morocco inatarajia kufanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, na Jumamosi itafanya mazoezi yake ya mwisho kwenye
Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa saa 9 kamili alasiri.

Wachezaji walioko kwenye kikosi hicho chini ya Kocha Rachid Taoussi ni
Nadir Lamyaghri, Anas Zniti, Yassine Bounou, Younnes Bellakhadar,
Abdellatif Noussair, Abderrahim Achchakir, Zoheir Feddal, Younnes Hammal,
Zakarya Bergdich na Abdeljalil Jbira.

* *

Issam El Adou, Kamel Chafni, Salaheddine Saidi, Mohamed Ali Bamaamar,
Abdelaziz Barrada, Salaheddine Aqqal, Abdessamad El Moubarky, Nordin
Amrabat, Chahir Belghazouani, Abdelilah Hafidi, Youssef Kaddioui, Brahim El
Bahri, Hamza Abourazzouk na Youssef El Arabi.

Wakati huo huo, tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa keshokutwa
katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo,
mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha
Mafuta Buguruni, Uwanja wa Taifa na Dar Live Mbagala.

Milango siku ya mechi kwa ajili ya watazamaji itafunguliwa saa 6 kamili
mchana.

20130320-082134.jpg

Comments