Man United juu kwa pointi 12

*Aston Villa sasa waona mwezi

Manchester United wamezidi kuwaweka pabaya mabingwa watetezi, Manchester City, baada ya kupaa kileleni mwa ligi kwa tofauti ya pointi 12.

United waliokuwa wakiongoza ligi kwa tofauti ya pointi tisa, wameongeza nyingine tatu kwa kuwachaoa Everton mabao 2-1.

Manchester City wamebaki wakijilaumu kwa kuweka kombe rehani, baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 Jumamosi kutoka kwa Southampton.

United wamewafunga Everton ambao miezi tisa iliyopita walilazimisha sare ya 4-4 hapo hapo Old Trafford, na kuwa chanzo cha kupoteza ubingwa wao.

United walipata mabao yote mawili katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Ryan Gigs na Robin van Persie na kuwaweka United mahali pazuri pa kutwaa taji la ubingwa kwa mara ya 20 mwaka huu.

Giggs amepiga hatua kubwa binafsi, kwani sasa ameshafunga katika misimu 23 mfululizo ya ligi ya soka.

Everton walipambana vilivyo, lakini Phil Jones alifanikiwa kumzuia mpachika mabao wao mrefu na mwenye nguvu, Maroune Fellaini.

Kwa kufungwa huko, Everton sasa wameachwa nafasi ya sita, nyuma ya Arsenal, Tottenham Hotspurs, Chelsea, Man City na United wanaoongoza.

Katika mechi nyingine, Aston Villa wamefanikiwa kujiondoa kwenye eneo la kushuka daraja, baada ya kuwachapa West Ham United mabao 2-1.

Baada ya kucheza hovyo kipindi cha kwanza, Villa walibadilika kipindi cha pili na kufanya mashambulizi makali langoni mwa wapinzani wao.

Walipata bao la kwanza kwa penati iliyofungwa na Christian Benteke, baada ya Mark Noble kumchezea rafu Charles N’Zogbia aliyekuwa anakwenda kumwona golikipa.

N’Zogbia alifunga mwenyewe bao la pili, baada ya kutumbukiza wavuni moja kwa moja mpira wa adhabu nje ya 18.

West Ham walipata bao la kufutia machozi katika dakika za lala salama kupitia kwa Ashley Westwood, na kufanya dakika za mwisho kuwa za vuta nikuvute.

Kocha Paul Lambert wa Villa alionekana kujawa wasiwasi, kwani ni zaidi ya mara moja timu yake iliachia uongozi na ama kufungwa au kutoka sare.

Huu ni ushindi wa tatu tu nyumbani kwa Villa msimu huu, lakini umuhimu wake ni kwamba umewaondoa eneo la kushuka daraja, wakiwa nafasi ya 17.

Enhanced by Zemanta

Comments