Basketball Clinic kwa Msaada wa tanzaniasports.com Arusha.

                                                                                                                                           
 
Kwa niaba ya Shirikisho la mpira wa kikpu Tanzania (TBF) tunayo furaha kuwatangazia kuwa tutaendesha mafunzo maalumu (Basketball Clinic) ya vijana chini ya miaka 17 itakayofanyika Arusha tarehe 9-10 Juni, 2012.

 

Mafunzo haya yataendeshwa mmoja wa makocha bora sana wa kikapu duniani  anayetokea Marekani anaitwa Greg Brittenham, ambaye ni alikuwa kocha msaidizi kwa miaka 20 wa timu ya NBA inayoitwa New York Knicks ya Marekani, kocha huyo tayari yuko nchini.

 

Mafunzo haya yamewezekana kupitia Mtanzania anayeishi Uingereza Israel Saria  mmliki wa http://www.tanzaniasports.com/./ambaye ndie aliyetusaidia kumpata Kocha huyo. Habari zaidi za kocha huyo soma hapa: http://www.nba.com/coachfile/greg_brittenham/index.html au http://www.wakeforestsports.com/sports/m-baskbl/spec-rel/082611aaa.html

 

Kuwezesha mafunzo haya tumesaidiwa na watu wa Marekani kupitia ubalozi wa Tanzania ambao wametoa mipira na fedha za uwezeshaji na Kampuni ya Cocacola ambao nao wametoa mipira na vinywaji kwa vijana watakaoshiriki mafunzo hayo na kocha Greg ametoa fulana kwa vijana wote 100 na pia amejitolea kufanya mafunzo haya bila malipo, tunawashukuru sana.

 

Vijana watakaoshiriki mafunzo haya ni 100, kati ya hao wasichana ni 30 na wavulana ni 70 na wote ni wanafunzi wa shule mbali mbali kutoka jiji la Arusha na niji jirani.

 

Tunawashukuru walimu, wazazi na wadau wote wanaoshirikiana nasi kufanikisha mafunzo haya.

Tunaomba wakazi wa Arusha na maeneo jirani wafike kwa wingi katika viwanja vya Soweto amboko ndiko mafunzo haya yatafanyika kwa siku 2 kuanzia saa 3 asubuhi  hadi saa 9 alasiri.

 

TBF kwa kushirikana na wadau wetu tuliowataja hapo juu na wengine tutendelea kuendesha mafunzo kwa vijana wetu wadogo nchi nzima ili tuwajengee msingi mzuri nan i matumaini yetu kati ya hawa baadhi yao watakuwa ni wachezaji mashuhuri siku za baadae.

 

PHARES MAGESA

MAKAMU WA RAIS-TBF                                                                                

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments