Rais J. M. Kikwete na wanamichezo..

Pamoja na kuwa ratiba ya Rais wa nchi yeyote duniani kuwa ngumu kukutana na wale wote wanaopenda kukutana naye, kwa Rais Jakaya Kikwete, ni tofauti kidogo. Alipokuwa London hivi karibuni kwa safari ya kikazi tulipata nafasi mimi na mwenzangu Mariam Komanya kumsalimia Mhe Rais Jakaya Kikwete. Kwa kuonyesha kuwa anatukumbuka, alianza kwa kumuuliza Mariam…”Hujamaliza shule tu…..

Nami akaniuliza vipi Arsenal? kwa kuelewa kuwa mimi nina mapenzi na timu ya Arsenal, na baadaye nikamuuliza Mhe Rais, kama anasikiliza kipindi cha ulimwengu wa soka, kinachotangazwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC toka London, ambapo mimi ni mmoja wa wachambuzi wa masuala ya michezo ya kipindi hicho, akajibu ndio nawasikiliza sana, na kufuatilia masuala ya michezo mnayotangaza.

Kwa hakika tulifarijika sana, na kuona fahari kuwa Mtanzania nje ya nchi yako na rais wako anapata muda wa kujua kile unachokifanya.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments