Twiga Stars yatinga nusu fainali COSAFA

Timu ya taifa ya soka ya wanawake, Twiga Stars, imetinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (COSAFA), baada ya kuifunga Zambia 2-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Gwanzura hapa Zimbabwe.

 

Kwa ushindi huo, Twiga Stars imefikisha pointi sita baada ya juzi Jumamosi kuwafunga Botswana 3-1.

Twiga sasa itacheza mechi ya mwisho ya hatua ya makundi ya kukamilisha ratiba dhidi ya Afrika Kusini Jumatano.

Katika mechi ya jana, Twiga, ambayo imealikwa katika michuano hiyo baada ya kufanya vyema katika michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wanawake iliyofanyika nchini Afrika Kusini mwaka jana, magoli yote mawili yalifungwa na mshambuliaji Asha Rashid ‘Mwalala’ katika dakika za 21 na 33.

Mechi za hatua ya nusu fainali zitachezwa Alhamisi Julai 7

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments