Hatimaye Umitashumta yaanza kibaha!

Baada ya kimya cha muda mrefu hatimaye michezo ya umitashumta iliyoanza tarehe 14/12/2010 katika Kituo cha Elimu Kibaha.Ufunguzi ulifanywa na Waziri wa Nchi TAMISEMI MH George Mkuchika (Mb).Waliohudhuria ni pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh Shukuru Kawambwa.(Mb)Mwingine aliyehudhuria ni Naibu Waziri Tamisemi (Elimu) Mh Kassim Majaliwa (Mb).

Kwa mwaka huu mikoa 10 ndiyo itakayoshiriki. Mikoa hiyo ni Singida, Dodoma, Tanga, Iringa, Arusha, Morogoro, Pwani, Dar es salaam, Mbeya  na Kilimanjaro. Michezo iliyoshirikishwa mwaka huu ni mitatu ambayo ni Mpira wa miguu,Netball na Riadha.

Michezo inatazamiwa kufungwa tarehe 21/12/2010.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments