Arsenal kujaribu kumaliza uteja kwa Chelsea

Cesc Fabregas, cropped
Image via Wikipedia

KLABU Chelsea na Arsenal zinakutana kwenye Ligi Kuu zote zikiwa na kumbukumbu mbaya ya kipokea vipigo katika michezo yao iliyopita.

Pamoja na kuwa mahasimu hao wa London katikati ya wiki walipata ushindi mnono kwenye Ligi ya Mabingwa, lakini ushindi kwenye mechi ya leo ni muhimu zaidi kwao katika kurudisha matumaini yao ya kusaka ubingwa wa ligi ya England.

Mabingwa watetezi Chelsea walilala 1-0 kutoka kwa Manchester City, huku Arsenal akipokea kipigo cha mabao 3-2 nyumbani kutoka kwa timu iliyopanda daraja msimu ya West Bromwich Albion ikiwa ni pigo kubwa kwao.

Chelsea bado waonaongoza ligi hiyo pamoja na kufungwa, lakini Manchester United iliyo nafasi ya tatu itacheza na Sunderland leo na City watakuwa wenyeji wa Newcastle siku inayofutwa, kama Arsenal itafungwa itakuwa kwenye nafasi kubwa ya kuondelewa kwenye nne bora kesho.

Kipa Lukasz Fabianski alichukua nafasi ya Manuel Almunia Jumanne waliposhinda 3-1 dhidi ya Partizan Belgrade baada ya Mhispania huyo kufanya uzembe dhidi ya West Brom. Fabianski aliokoa penalti na anaweza kuendelea kudaka leo dhidi ya Chelsea.

“Ilikuwa ni pigo kubwa tulipofungwa Jumamosi, lakini nafikiri mmeona tulivyocheza dhidi ya Partizan ilionyesha kwamba tumejifungza kutokana na kipigo hicho,” alisema Fabianski. “Kiwango kile ni ishara tosha kwamba sasa tumejiandaa vizuri dhidi ya Chelsea.

“Itakuwa ni moja ya mechi nzuri ambazo watu wengi watapenda kuitazama.”

Arsenal itawakosa nyota wake majeruhi Cesc Fabregas, Theo Walcott, Robin van Persie na Nicklas Bendtner ambao hawakucheza mechi mbili zilizopita, kukosekana kwa wachezaji hao inaweza kuwa pigo kwao mbele ya  Blues.

Fabregas anasumbuliwa na matatizo ya nyama za paja tangu Sept. 18 na kocha Arsene Wenger amejindaa kuchangua bila ya kuwepo kwa nahodha huyo.

Enhanced by Zemanta

Comments