Kocha mpya Taifa Stars afurahia kuivaa Misri

Kocha mpya wa timu ya taifa ya soka, Taifa Stars, Mdenmarak Jan Poulsen, alisema amefurahishwa na taarifa kuwa timu yake itacheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Misri itakayopigwa Agosti 11 jijini Cairo, Misri.
Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam juzi usiku, Poulsen alisema kwamba amefurahia kuwepo kwa mechi hiyo kwani itampa nafasi ya kuwajua vizuri wachezaji wake.
Kocha huyo aliongeza kwamba, mechi hiyo pia itampa nafasi ya kujua namna atakavyokabiliana na Algeria katika mechi ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon na Equatorial Guinea mwaka 2012, kwani anaamini kuwa soka la ‘waarabu’ hao wa Afrika ya Kaskazini lifanana.
Licha ya kuifurahia mechi hiyo dhidi ya Misri, Poulsen atakumbana na kibarua kigumu kwani rekodi zinaonysha kuwa katika mechi ya mwisho baina ya timu hizo, Stars ilikula kipigo cha 5-1 kutoka kwa ‘mafarao’ hao, goli la Stars likifungwa na John Bocco.
Wakati huohuo, Poulsen ambaye jana alikuwepo pia kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Yanga ikiwaadhibu Telecom Wanderers kwa kipigo cha 4-1, atakutana na waandishi wa habari wiki hii na kuelezea mikakati yake ya kuiimarisha Stars.
CHANZO: NIPASHE
Enhanced by Zemanta

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments