Timu inaendelea vizuri na mazoezi nchini Uingereza

Hali ya wachezaji:

Wachezaji wote tisa ni wazima wa afya ukiacha upungufu wa wachezaji Watatu kuwa na maumivu ya miguu na kuwafanya kucheza kwa vipindi vichache vichache . Wachezaji wenye matatizo ya kuumia ni Lilian Sylidion (Misuli) na Semeni Mathew (Nyayo) na Paskalia Kibayasa (Nyongo). Pamoja na kuumwa kwao lakini wamendelea na mazoezi kwa taabu kwani tunaupungufu wa idadi ya wachezaji walioweza kusafiri na timu. Wachezaji tulikojua nao ni Tisa na mchezo huchezwa na wachezaji saba hivyo. Hivyo tunatatizo la wachezaji wa akiba kutokana na wachezaji watatu kuwa majeruhi. Hatukuweza kuja na idadi kubwa ya wachezaji kwa sababu kubwa mbili: (1) Uhaba wa fedha za kusafirisha wachezaji wengi kwani safari inagharimu Tsh. 3.2 kwa mchezaji mmoja) (2) Wachezaji wawili walichelewa kupata Viza hivyo tukawaacha iki wakipata watufuate lakini hadi sasa bado hawajafika (Veronica Patrick na Mpala Iddi toka Jeshi la Wananchi la Tanzania)

Mazoezi:

Tumekuwa na mazoezi na waalimu wa kimataifa toka nchini Uingereza na kufanya mazoezi ya pamoja na timu na wachezaji wa kimataifa wa Uingereza. Mazoezi ni mazuri sana hasa ukizingatia kuwa tunajifunza kwa vitendo na kufanyia mazoezi kwa vitendo na watu walio bora. Mazoezi yamehusisha sana : Mbinu na Maarifa ya Mchezo kwa mchezaji, Uimarishahi wa mwili wa mchezaji na Mifumo mbalimbali ya kucheza  kama timu.

Michezo ya kirafiki:

Hadi sasa tumecheza michezo miwili ya kirafiki, matokeo yakawa kushinda mchezo mmoja na kushindwa mchezo mmoja. Hakika Michezo hii imekuwa na manufaa sana kwani ni migumu na vijana wanacheza kwa usimamizi wa kutakiwa kucheza kutokana na walivyofundishwa ili kurahisisha kubadilika chini ya usimamizi wa waalimu wa huku. Pia vijana wanalazimika kucheza wakiwa na wenzao majeruhi kwani hawana watu wa kubadili.

Matokeo ya michezo

Tarehe 8/4/10: Tanzania vs Leeds City Combine (Leeds Metropolitan) : TZ: 28/ Leeds: 63

Tarehe 9/4/10: Tanzania vs Bradford City Combine (North West Jays): TZ: 50/ Bradford: 36

Tathimini:

Kiwango cha matumizi ya ujuzi na maarifa ya mafunzo mchezoni ni Mkubwa na wa haraka kwa timu ya Tanzania kwa maelezo ya waalimu wanaoifundisha timu.

Matukio mengine:

Tarehe 9/4/10: Timu ilikaribishwa rasmi katika jiji la Bradford na Mayor wa Jiji la Bradford kwa taafrija ya chakula cha mchana. Afisa Msaidizi wa Balozi wa Tanzania (Bwana Allen Kuzilwa) alikuwepo kuwakilisha ubalozi wa Tanzania. Ghafla ilikuwa nzuri sana na wangeni wengi mashuhuri toka katika jiji la Braford walihudhuria na timu ilipata nafasi ya kutembelewa maeneo ya kumbukumbu mbalimbali za kitaifa za nchi ya Uingereza.

Mazungumzo ya awali yalifanyika baina viongozi wa timu ya Tanzania, chuo cha Braford (Bradford College), Shirikisho la Mchezo wa Netiboli Duniani juu ya Wazo la kuanzisha uhusiano rasmi kwa michezo na elimu baina ya Tanzania (kupitia Netball) na chuo cha Bradford pia Uhusiano na Jiji la Bradford. Mazugumzo yataendelea katika hatua ya pili ambapo ubalozi wa Tanzania utahusishwa.

Leo tarehe 10/4/10 timu inaendelea na mazoezi ya darasani na vitendo katika mji wa Bradford. Tayari timu imetembelew miji ya Manchester, Sheffield, Leeds na Bradford.

Watanznaia wanaosoma katika chuo cha Bradford wapatao sita walijumuika nasi katika mchezo wa jana na leo wameandaa chakula kwa ajili ya timu. Tunapenda kuwashukuru sana kwa moyo wao wa upendo.

Scotland:

Timu itaondoka kesho tarehe 11/4/10 kuelekea nchini Scotland kwa mwaliko wa Netball Scotland na kutembelea miji ya Glasgow na Edinburgh kwa mazoezi na kuchezo michezo ya kirafiki hadi tarehe 17/4/10 itakaporejea nyumbani.

Joel Mwakitalu

Mratibu wa Safari

Jijini Bradford

On Behalf of:

Tanzania Netball Association – CHANETA

P.O. BOX 60240, Dar es Salaam

Tel: +255 732 994587/654 209954 – Office

Tel: +255 754 613651 – Chairman

Tel: +255 754 297830 – Secretary General

Fax +255 22 2420178/22 2850972

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments