TFF ZINDUKENI

Kuna semi nyingi za Kiswahili zimesheheni busara ,maarifa na hekima za wazee wetu.

Kwa ufupi semi hizo ni kama wosia kwetu na vizazi vyote vijacho.

Bila shaka sote tunafahamu kuwa kila mmoja wetu ana mapungufu ya namna moja au nyingine. Hali hiyo basi inafanya watu kurekibishana na hata wakati mwingine watu hao kuingia katika migogoro isio na sababu za msingi.

Wanadamu kwa ujumla tuna tabia ya kutothamini vitu tunavyoishi navyo katika maisha yetu ya kila siku. Viwe vya majumbani mwetu au vya maofisini. Moja ya sababu ya kasoro hii ni kule kuvioona wakati wote na kuzoea kuvitumia.

Kuna msemo usemao mazoea yana tabu. Kwani mazoea yana tabia ya kujenga utandu machoni mwetu na pazia katika akili hata kufikia kikomo cha kutuoona wala kuthamini umuhimu wa vitu hivyo

Umuhimu wa wa vitu tunavyoishi navyo huendelea kuchujuka na kupauka kadri tunavyoendelea kuwa navyo

Ukweli nimetangulia kuandika makala haya kwa semi hizo hili kutia mkazo maana pana na ya  kina kirefu ya  tungo hizo za wazee wetu.

Hivi karibuni nilitembelea ofisI za Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini- TFF.

Sikuweza kuamini macho yangu. Mathalani  jengo linalofanyiwa mikutano na waandishi  yaani Press conference room. Hali ya hicho chumba hairidhishi hata kidogo.Licha ya kuwa na waya za umeme zinazonigania ovyo  pia kimegubikwa na matanda bui ovyo

Kwa  upande wa GYM hali nao sio nzuri haswa katika usafi.

Sina uhakika mara ya mwisho chumba hicho kilitumika lini lakini kuna haja ya kuvitunza vifaa hivyo. Hata kama mlipewa bure bado TFF mnawajibika kwa niaba yetu sisi wadau

Jengo lililonitia huzuni ni ile hostel ya vijana wetu pale Karume. Nilishangazwa na kitendo cha Shirikisho hilo kupuzia kabisa huduma ya hosteli.Vyumba vya hostel sio visafi , vitanda na magodoro yako katika hali mbaya sana. Nilikuwa na mawazo kuwa kumiliki vitu hivyo kwa Shirikisho letu litawapunguzia gharama kubwa ya kiundeshaji kwa kuwaweka wachezaji wetu kambini hapo wakati wa maandalizi.

Tupende tusipende usafi na matengenezo madogo madogo kamwe hautaji  fedha toka FIFA- Shirikisho la mpira Duniani.. Labda kupuzia majengo yao ni kutokana na kazi nyingi au kuwa na kasoro kama nilizozingumzia hapo awali .

Bahati nzuri Shirikisho hilo ni baadhi ya Taasisi za michezo nchini zinazopata fedha nyingi kujiendesha katika shughuli zake za siku hadi siku

Kuhusu kazi , siaamini kuwa Shiriksho hilo lina kazi nyingi na kupuuzia majengo yao

Mathalani kuhusu kuendesha Ligi  ni kuwa nchi pekee Duniani  tunaoendesha Ligi ya daraja mbili tu yaani VODACOM PREMIER LEAGUE na LIGI DARAJA LA KWANZA. Bahati mbaya sifahamu nani anaendesha ligi daraja la pili hadi la nne kama lipo. Kwa mfumo tunavyoendesha ligi zetu basi kuna hatari ya kudumaa kisoka na kama alivyowahi kusema mmoja ya walimu wa mchezo huo nchini :Hata aje Ferguson  kuendelea kwa soka letu bado litakuwa tatizo kutokana na kutokuwa na msingi imara .

Pamoja na mengi mazuri mnayoendelea kuyafanya tangu muingie madarakani  bado kuna haja kubwa ya Kuzinduka na kulindesha Shirikisho hilo kisasa  na kwa ufanisi zaidi.

Posted under:  All Articles

Tags:  

Comments