Kenya, Tanzania kuandaa fainali za Afrika 2014

SHIRIKISHO la Soka Kenya, KFF limeomba Shirikisho la Soka Afrika uenyeji wa Fainali za Afrika 2016 na kuiteua Tanzania na Uganda kuunganisha nguvu kuandaa kwa pamoja.

Taarifa ya KFF ambayo Mwananchi imeipata, ilisema kuwa kwa muda mrefu shirikisho hilo limepeleka maombi CAF kutaka uenyeji huo huku likijinadi kujitosheleza kwa miundombinu.

“Baada ya mkutano wetu kwa pamoja, Job Omino (mwenyekiti wa taifa), Sam Obingo (katibu) na James Tirop kwa mara ya kwanza tuliomba haya kwa Fainali za 1996. Hata hivyo, Afrika Kusini ndiyo ilikuwa mwenyeji.

Hata hivyo, serikali kupitia kwa Waziri wa Michezo, James Njiru alipinga hatua hiyo ya KFF lakini baada ya ujio wa wawakilishi kutoka shirikisho la soka Afrika CAF na kuishauri Serikali umuhimu wa kuandaa michuano hiyo wengi walikubaliana na kauli hiyo ingawa wengine walipinga lakini shirikisho hilo likasimama na kutetea nafasi hiyo.

KFF haikukata tamaa na ilibidi kuwasilisha michoro ya viwanja ikiwemo wa Mombasa, Moi Kasarani na City na CAF iliridhishwa na hatua hiyo na kuitaka Kenya kuendelea kujipanga.

Baadaye CAF ilimtuma mjumbe wake, Farah Addo kwenda kikagua viwanja pamoja na kuwa na mazungumza na Waziri wa sasa wa Michezo, Maalim Mohamed na katika mazungumzo yao, walizungumzia jinsi gani wanaweza kuufanyia ukarabati Uwanja wa Mombasa ambao nao ungeweza kutumika kwa fainali hizo.

Sasa, pamoja na kwamba Afrika Kusini inataka kuwa mwenyeji wa Fainali za 2016, lakini tangu kuingia kwa Job Omono katika Chama cha FORDKENYA mpango wake ni kuunganisha kupitia soka ambao morari ya soka imepotea.

“Tunataka kuandaa Fainali za 2016 na endapo inashindikana, mpango wetu ni kuandaa kwa pamoja na Tanzania, Uganda na Zanzibar,” ilisema taarifa ya KFF.

CAF wasiwe na wasiwasi na Kenya kama tukishinda,

lazima Bunge liidhinishe fedha ili vijengwe viwanja vitatu vya kisasa na pia lazima itolewe barua ya idhini ya Rais kuruhusu fainali hizo bila kujali yeyote atakayeshinda urais katika uchaguzi wa 2012.

Hata Kenya ikikosa kama Kenya lazima ujumbe wa Afrika Mashariki kupitia Rais wa TFF na CECAFA, Leodegar Tenga lazima kuipenyeza na kuipigia debe hoja ya Afrika Mashariki kuwa mwenyeji wa Fainali za 2016.

CAF inaweza kuangalia wazo la kuandaa kwa pamoja nchi za Afrika Mashariki kwa kuwa kila nchi tajwa kuna viwanja vya kisasa katika miji ya Nairobi, Dar es Salaam na Kampala. Zanzibar inaweza kutumika pia.

Timu 16 zitagawanywa katika mataifa manne ya Afrika Mashariki na mechi tisa zitachezwa kila nchi hatua ya makundi, pamoja na mechi za robo fainali zitachezwa katika miji ya Nairobi, Kampala, Dar es Salaam na Zanzibar.

Mechi za mshindi wa tatu, nusu fainali na fainali zitafanyika katika nchi ambazo waandaaji watakubaliana kati ya Nairobi, Dar es Salaam na Kampala.

Mawasiliano ni mazuri Afrika Mashariki, viwanja bora vinavyohitaji ukarabati mdogo, vivutio vya utalii, hoteli za kisasa, mashabiki wanaweza kusafiri kwa barabara kwenda kwenye mechi bila vikwazo.

Wakati huo huo, CAF imesema kuwa mechi za ufunguzi kwa Fainali za Afrika 2012 zitakazoandaliwa kwa pamoja kati ya Gabon na Guinea ya Ikweta itachezwa Guinea ya Ikweta wakati fainali itachezwa Gabon.

Comments